
Mshambuliaji Emmanuel Okwi
Akizungumza kuelekea mchezo wa ligi kuu, Ndanda Fc dhidi ya Simba utakaompigwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara hii leo, Okwi amesema,
“Mimi ningependa kusema kama ninavyosema kila siku, kwanza naangalia maslahi ya timu, nahakikisha timu inafanya vizuri na nikifanikiwa kufunga magoli katika mchezo wa leo itakuwa vizuri zaidi lakini mimi sina wasiwasi wowote wa kufunga magoli ishirini kama nilivyofanya msimu uliopita, ni kuhakikisha kuwa nafanya vizuri”.
Simba ina historia nzuri dhidi ya Ndanda Fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona tangu Ndanda Fc ilipopanda daraja kwa mara ya kwanza msimu wa 2016/17.
Mpaka sasa timu hizo zimekutana mara tatu katika uwanja huo, ambapo Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yote, ikishinda kwa mabao 2-0 Januari, 2015, pia ikaibuka na ushindi wa 1-0 mwezi Januari mwaka 2016 na ushindi wa 2-0 msimu uliopita.
Simba inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo hasa kutokana na safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho msimu huu, kilichoongezewa nguvu na mshambuliaji raia wa Rwanda, Meddie Kagere ambaye ana mabao matatu mpaka sasa katika michezo miwili aliyocheza.