Tuesday , 28th Aug , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Bright anatarajia kuitwa baba hivi karibuni kwa kile kinachodaiwa kuwa mpenzi wake Brandy ambaye ni binti wa Rais wa muziki wa dance bongo, Nyoshi Al-Sadati, kuwa na ujazuzito wake.

msanii Bright

Hayo yamebainika wakati Bright alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya msanii huyo kukutwa akiwa 'Super Market' na mpenzi wake wakifanya manunuzi ya vitu mbalimbali kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.

"Super Market ni eneo ambalo anaenda mtu yoyote kununua kitu ambacho anahitaji, kwa hiyo sidhani kama kuna kingine kinafanyika. Suala la ujauzito halijifichi kwa hiyo muda ukifika chochote kinaweza kikatokea", amesema Bright.

Pamoja na hayo, Bright ameendelea kwa kusema "mimi na Nyoshi tunafahamiana sana tu, labda yeye hanifahamu mimi kwa suala la fedha, lakini ninaamini anafahamu kama mimi ndio mkwe wake".

Mtoto wa Nyoshi (Brandy)

Kauli hizo za Bright zimekuja baada ya kupita siku chache tokea, baba mzazi wa Brandy ambaye ni Nyoshi kusema hashangai kusikia binti yake kuingia katika mahusiano licha ya kuwa na umri wa miaka 18 ambapo kwa sheria za nchi ni bado mtoto mdogo kujihusisha na masuala kama hayo.

Mtazame hapa chini Bright akifunguka juu ya jambo hilo.