Tuesday , 1st Jul , 2014

Maandalizi ya michuano ya mchezo wa Gofu ya kuadhimisha miaka 50 ya JWTZ yameanza kwa wachezaji wa mchezo huo kujinoa katika viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam.

Maandalizi ya michuano ya mchezo wa Gofu ya kuadhimisha miaka 50 ya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ yameanza kwa wachezaji wa mchezo huo kujinoa katika viwanja vya Gofu vya Lugalo jijini Dar es salaam mashindano ya yanayotarajia kuanza Septemba 30 na 31 mwaka huu.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo Mwalimu wa Gofu katika viwanja hivyo Japhet Masai amesema tayari wachezaji wa Gofu walio ndani ya jeshi na walio nje ya jeshi wanajinoa ili kuhakikisha wanaibuka katika mashindano hayo.

Masai amesema licha ya kuwepo kwa michezo mbali mbali lakini katika mchezo wa gofu kuna zaidi ya wachezaji 50 watakaotoka nchi za Afrika Mashariki ambao watashiriki na hivyo kuleta ushindani mkubwa na kuwa kivutia kwa watazamaji watakaofika kushuhudia mashindano hayo.