Wednesday , 25th Jun , 2014

Mchekeshaji mahiri kutoka tasnia ya filamu hapa Bongo, Mboto Haji leo hii ameshiriki kuchat Live na mashabiki wake kupitia Kikaangoni Live ya ukurasa wa facebook wa EATV, ambao unahusisha familia kubwa kabisa ya mashabiki zaidi ya laki 3.

Mboto Haji kupitia nafasi hii, ameweza kuweka wazi mambo mengi kwa mashabiki wake kuhusiana na sanaa yake na hata maisha yake binafsi kwa njia ya kujibu maswali ambayo ameulizwa moja kwa moja na mashabiki hao mtandaoni.

Katika zoezi hilo la Kikaango Mboto ameongea na enewz akisema kuwa amefurahishwa sana kupata nafasi hiyo kubwa ya kuchat na mashabiki wanaofuatilia kazi zake na kuguswa na maswali mengi likiwepo la kuhusu kama yeye ana mahusiano na demu yeyote.

Mboto katika kuliweka sawa swali hilo alipenda kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye hana demu bali ana mpenzi wake anayempenda pamoja na mtoto mmoja, pia kuhusu swali la kuoa amesema kuwa swala hilo halihitaji haraka ni lazima kwanza ujipange.

Kumbuka kuwa zoezi hili la Kikaangoni Live linafanyika kila Jumatano saa 6 mpaka saa 8 mchana kupitia www.facebook.com/eatv.tv, like ukurasa huu kama bado hujafanya hivyo ili kuwa sehemu ya familia hii kubwa, na kaa tayari kwa staa mwingine mkali kupitia Kikaangoni Live wiki ijayo.