
Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa Kayembe amekuwepo nchini akifanya majaribio kwa muda mrefu chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina.
Usajili wa Kayembe sasa unazima uwezekano wa beki wa klabu hiyo Mtogo, Vincent Bossou kurejeshwa Jangwani. Bossou alimaliza mkataba wake msimu uliopita baada ya kuitumikia Yanga kwa miaka miwili alitarajiwa kuendelea kutokana na kufanya vizuri.
Usajili wa Kayembe unakuja muda mfupi baada ya Yanga kuruhusu goli la tano kwenye ligi kuu msimu huu ambalo lilipelekea timu hiyo kulazimishwa sare ya 1-1 na Tanzania Prisons jana jioni.