Friday , 23rd May , 2014

Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuto kata tamaa na kuona kwamba teknolojia ya sayansi ni vitu visivyowezekana katika kujiajiri, badala yake kufanya jitihada na kuelekeza nguvu zao kwenye kusomea masomo hayo.

Mkurugenzi mkuu wa tume ya taifa ya sayansi na teknolojia, Dkt Hassan Mshinda (kushoto), akiwa na afisa habari wa tume hiyo Theophil Pima (katikati) wakiwa katika mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari hivi karibuni.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Afisa Habari wa Tume ya taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini COSTECH Bw.Theophili Pima wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio namna tume hiyo inavyowawezesha vijana katika kujiajiri.

Amesema mpaka sasa tume hiyo imeshawawezesha jumla ya vijana 500 kuweza kujiajiri katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kutumia mifumo mbali mbali ya sayansi na Teknolojia na hivyo bado vijana wana nafasi ya kutumia fursa hiyo kwa lengo la kujiajiri kukuza kipato chao.