
Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambazo bado hazijathibitishwa, zimesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na ratiba ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
EATV imemtafuta Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ambaye amesema kuwa taarifa hiyo bado haijamfikia mezani, na kusema kuwa taarifa rasmi itatoka kesho (Jumanne).
"Taarifa hiyo haijafika kwangu, bado sijaambiwa kitu, nikipewa taarifa nitazitoa, tusubiri kesho" Amesema Lucas
Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya FC katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.