Monday , 12th Dec , 2016

Leo ni siku ya Mapumziko ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W), ambapo waislamu nchini wametakiwa kuzingatia maadili wanapokuwa sehemu zao za kazi ili waweze kutenda haki kwa wananchi bila kujali itikadi zao.

maulid katika viwanja vya Maisara Unguja

 

Hayo yamezungumzwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Musa Salum kwenye sherehe za mauli zilizosomwa jana usiku ambapo waislam wanasherekea kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W).

Sheikh Alhad Salum amewataka waislam kuiga mwenendo wa Mtume wao kwa kuwa na maadili kwa kutenda haki kwa kila mtu pamoja na kukemea maovu yanayoendelea kushamiri ulimwenguni.

Sheikh Alhad Musa Salum - Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Pangani ambaye alihudhuria sherehe hizo, Bi. Zainabu Abdallah , amewataka wanawake kujitambua na kuwa mstari wa mbele katika kufanya kazi kwa bidii.