Monday , 12th Dec , 2016

Wapenzi, mashabiki na wadau wa burudani nchini wameelezea hisia zao kuhusu tukio kubwa la utoaji wa tuzo kubwa na za kwanza Afrika Mashariki, za EATV Awards, huku wengi wao wakionesha kukunwa na maandalizi ya tukio zima pamoja na kutoa ushauri

Maoni ya baadhi ya wadau

Watanzania hao wametoa hisia zao kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama inavyoonekana katika picha hapo juu, huku baadhi yao wakishauri kuwa wangependa kuona mwakani vipengele vinavyowaniwa vikiongezeka ili kunogesha zaidi mambo.

Baadhi yao wamesikitishwa kuona baadhi ya washindi wakikosekana siku ya tukio na badala kutuma wawakilishi jambo ambalo linapunguza utamu wa shughuli, lakini kiujumla wameonesha kukubali maandali ya ukumbi pomoja na mpangilio wa burudani ulivyo kuwa .

Sikiliza hapa maoni ya baadhi ya wapenzi wa burudani walioingia kwenye tukio.

 

Tags: