Thursday , 1st Dec , 2016

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage ametolea ufafanuzi gharama kubwa za makaa ya mawe yanayozalishwa nchini ikilinganishwa na yale yanayotoka nje ya nchi.

Charles Mwijage (kushoto) - Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji akiongea na wanahabari leo

Mwijage amesema hilo linatokana na kuwa makaa hayo yanasafirishwa kwa barabara njia ambayo ni ya gharama kubwa tofauti na yale ya Afrika Kusini ambayo husafirishwa kwa njia ya majini ambayo ni gharama nafuu.

Aidha, amewataka wananchi kutambua kuwa serikali inathamini mchango wa kiwanda cha saruji cha Dangote ambacho amesema kimeongeza ushindani katika soko na kushuka kwa bei ya saruji na kuongeza kuwa nchi kwa sasa haiwezi kukumbwa na uhaba wa saruji.