Saturday , 26th Nov , 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva, mwanadada Vanessa Mdee a.k.a Vee Money, amefunguka na kueleza faida alizopata kwa kuwa karibu na nyota wa muziki nchini Marekani Trey Songz.

vanessa Mdee katika FNL

Akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, Vanessa alitakiwa kueleza faida alizopata kutokana na skendo zilizovuma siku za hivi karibuni kuwa alitoka kimapenzi na Trey Songz kipindi walipokuwa nchini Kenya katika Coke Studio.

Katika majibu yake, Vanessa alisema kuwa hakuna jambo linalovuma kwake bila ya kuwa na faida, na kwamba skendo hizo zilivuma hadi Marekani, kwani aliandikwa katika baadhi ya blogs za Marekani kuhusu ukaribu wake na Trey Songz, kitu kilichomfanya kujulikana hadi katika taifa hilo lenye nguvu katika karibu kila nyanja, ikiwemo muziki duniani.

Vanessa akijiselfisha na Sam Missago katika FNL

 

Katika FNL ya Sam Misago ilikuwa hivi....... 

Swali: "Vipi ishu ya wewe na Trey Songz imekupa faida gani, je kuna Wamarekani wamekujua au imeishia hapa hapa?"

Jibu: "Yea, hakuna jambo naweza fanya bila manufaa, hiyo imenifanya niandikwe kwenye blogs kadhaa nchini Marekani, kwahiyo wamarekani wamenijua"

Trey Songz amekuwa akifananishwa kimuonekano na mpenzi wa Vanessa, Jux licha ya Jux mwenye kuweka wazi kuwa Trey Songz ndiye role model wake.

Trey Songz

Katika hatua nyingine Vanessa ameeleza furaha yake kuingia kwenye tuzo za EATV, na kuomba mashambiki kumpigia kura katika kipengelee cha Mwanamuziki Bora wa Kike.

Kumpigia Kura Vanessa na wasanii wengine ingia hapa:- https://www.eatv.tv/awards

Tags: