
Sheikh Abubakar Zubeir - Mufti Mkuu wa Tanzania
Akiongea na vyombo vya habari jijini Dar es salaam, Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zubeir amesema Maulid ya mwaka huu yataadhimishwa kwa namna tofauti ambapo waumini wa kiislamu kote nchini watatakiwa kuchangia damu na kufanya zoezi la usafi katika maeneo yao mara tu baada ya ibada.
“Kipenzi chetu Mtume Muhammad amesema “Uislamu ni Usafi basi jisafisheni kwani hakika hataingia peponi isipokuwa Msafi, mwa misingi hii mimi mwenyewe nitaongoza usafi kufurahia kuendana na kuiga na kutekeleza mafundisho yake” amesema.
Aidha, amewataka viongozi wa baraza kusimamia na kuhimiza amani ya nchi yetu na kutokuwa tayari kuwavumilia wale wote ambao wanataka kuharibu amani na utulivu katika nchi yetu.
Kauli mbiu ya Maulid ya mwaka huu ni "Muislamu jitambue badilika amani na usalama ndiyo maisha yetu”
Ambapo amesema kuwa ni jukumu la kila muumini wa dini ya kiislamu na waumini wa madhehebu mengine kutunza amani. amesema.