Tuesday , 22nd Nov , 2016

Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na sekta binafsi kwa kuwa sekta hiyo inatoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo ya taifa.

Uledi Musa

 

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Uledi Mussa alipozungumza na East Africa Radio kuhusu ofisi ya waziri mkuu inatoa tathmini gani juu ya utekelezaji wa maswala yaliyopewa kipaumbele kwenye sera ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

Amewaomba wadau wa sekta binafsi kushirikiana na serikali kwakuwa serikali inawaunga mkono kwani sekta hiyo ndiyo inatoa ajira nyingi zaidi ambazo walipakodi wake ndiyo wanaliongezea taifa mapato ya kila siku ambayo yanatumika kutimiza malengo ya nchi waliojiwekea.

Amesema serikali inafanya kila jitihada za kuhakikisha inashirikiana na sekta binafsi katika kuzalisha ajira nchini na wanaamini serikali ya awamu ya tano itawawezesha na kuwaboreshea mazingira yao katika uzalishaji