Sunday , 2nd Oct , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Oktoba, 2016 amemteua Bw. Laston Thomas Msongole kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Rais Magufuli

Bw. Laston Thomas Msongole anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Edmund B. Mndolwa ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi wa Bw. Laston Thomas Msongole umeanza leo tarehe 02 Oktoba, 2016.