
Waziri Jenista Mhagama akiwa ameambatana na uongozi wa NSSF alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni
Zaidi Mh. Mhagama ameziagiza Bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kuhakikisha wanawasukuma wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.
Waziri Mhagama ametoa maagizo hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni na kutumia fursa hiyo kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, Bw Erick Shitindi kuhakikisha uongozi wa mifuko hiyo unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote walioshindwa kulipa madeni yao.
Awali, Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya mfuko wake kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na zile za binafsi wakiwemo pia wale walionunua nyumba za shirikal hilo.
Kwa mujibu wa Prof. Kahyarara, shirika hilo bado linadai takribani sh bilioni 20 kutoka kwa wa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za kimarekani milioni 1.2. Kiasi kingine cha bilioni 86 kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa waajiri walioshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao.