
Rais Bongo alipata asilimia 50.6 dhidi ya mpinzani wake, mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Afrika Jean Ping aliyepata asilimia 47.24.
Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho rasmi yaliotolewa na mahakama ya katiba Bongo alishinda na kura zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa katika ngome ya kiongozi huyo Haut-Ogoue.
Hatahivyo kura katika vituo 21 mjini Libreville zimefutiliwa mbali kutokana na ombi la upande wa kampeni ya rais. Na kutajwa kuwa sababu ya kiongozi huyo kupata asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho.
Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na kuiomba mahakama iamrishe kuhesabiwa upya kura hizo, katika eneo hilo la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ana wafuasi wengi.