Waziri Makuu Kassim Majaliwa
Majaliwa amesema hayo bungeni leo kufuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mlimba Bi. Suzan Kiwanga, aliyetaka ufafanuzi wa serikali katika kile alichoeleza kuwa ni kutoingizwa kwa vijiji vitatu katika utaratibu mzima wa uongozi, hali iliyoviathiri vijiji hivyo kibajeti kutokana na kudaiwa kuwa chini ya eneo la uwekezaji.
Katika maelezo yake, Mhe Waziri Mkuu amesema mchakato wa bajeti huanzia ngazi ya vijiji, kata, wilaya, mikoa na baadaye kwenye wizara, na kwamba mtiririko huu unatoa nafasi kwa kila ngazi kuandaa mpango wake wa kifedha na hivyo iwapo ngazi moja imeshindwa basi ngazi ya juu kabisa inawajibika kuandaa bajeti husika na kwamba suala la bajeti linawahusisha Watanzania wote.