Waziri wa nchi Ofisi ya rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mhe. George Simbachawene.
Waziri Simbachawene ametoa Onyo hilo wakati akihitimisha ziara yake ya Siku mbili Mkoani Songwe, ambapo amebaini kuwa miradi mingi ya maendeleo ya wananchi katika Halmashauri nyingi nchini imekwama kutokana na viongizi wengi hasa madiwani kuwa na makampuni binafsi na kujigawia zabuni.
Mhe, Simbachawene amesema utoaji wa Zabuni katika sehemu nyingi umejaa harufu ya rushwa na ubadhilifu na inatolewa kwa upendeleo na hata kwa watu wasiokuwa na sifa ya kuendeleza miradi na ndio maana miradi mingi inashindwa kumalizika.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa serikali ipo karibu na Halmashauri za Wilaya na mikoa Mipya ili kuweza kujimudu na kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wakazi wa maeneo hayo mapya ikiwa ni kuwafikishia huduma za kijamii katika maeneo yote yanayohitajika.
Simbachawene amesema licha ya serikali kupeleka fedha nyingi katika Halmashauri nyingi nchini kwa ajili ya miradi ya maendele lakini imeonekana fedha hizo zinapotea kutokana na usimamizi mbovu pamoja na viongozi wengi kuendekeza maslahi binafsi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Chiku Galawa amewataka viongozi wa mkoa huo kuchana na masuala ya siasa kwa sasa na badalae yake wajikite katika kuwahudumia wananchi kwa kufanya kazi na kuwapa huduma stahiki.