Wednesday , 8th Jun , 2016

Mbunge wa jimbo la Kalengo Mhe. Godfrey Mgimwa ameitaka serikali kurekebisha sheria za uwekezaji na kuondoa kero za mrundikano wa kodi leseni na gharama za uwekezaji ambazo kwa kiasi kikubwa zitaikwamishwa serikali katika azma yake ya uzalishaji na k

Akiongea na East Africa Radio katika mahojiano maalum Mhe. Mgimwa amesema Tanzania itawiwa vigumu kushindana na nchi za jirani katika uzalishaji hasa wa viwanda kwani sheria zake zinatafsiri ya kukataa wawekezaji ikizingatiwa kuwa hakuna nchi yoyote dunia ambayo inakataa wawekezaji.

Akitolea mfano katika jimbo lake la Kalenga Mkoani Iringa, Mhe. Mgimwa amesema kuna fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya uchimbaji madini, Kilimo, utalii ambavyo uwekezaji wa viwanda utawakomboa wakulima wa maeneo hayo pamoja na taifa kwa ujumla lakini kutoka na sheria mbovu uwekezaji umekuwa mdogo jimboni kwake.

"Kalenga kuna fursa za uwekezaji, katika sekta ya madini, utalii kilimo na maeneo mengine ya viwanda na uzalishaji mbalimbali, nivyema wawekezaji wakatumia fursa zilizopo kalenga kuwekeza, mazingira nimazuri"amesema Mgimwa

Mgimwa amesema ni vyema serikali ikadhibiti jambo hilo kwani inakosa wawekezaji na pesa za kigeni na taifa kubaki nyuma kwa kushindwa kushugulikia mambo madogo licha yakuwa na tija kubwa katika taifa.

Kwa upande mwingine Mhe. Mgimwa ametoa msimamo wake kwa kukwerwa na tabia ya Tanzania kuwa nyuma katika uuzwaji na kutangaza raslimali zake katika soko la kimataifa akitolea mfano Madini ya Tanzanite na Mlima Kilimanjaro ambazo zikitumiwa na mataifa mengine kujiingizia kipato.

"Unakuta ndege ya Kenya ina nembo ya mlima Kilimanjaro, Kenya inaongoza kwa kuuza madini ya Tanzinite kuliko sisi jambo ambalo linashangaza sana, hatuna ndege za kutosha kufanya safari nyingi za kimataifa nahii yote inapeleka tuna rudinyuma" Amesema Mgimwa

Mgimwa amesema umefika wakati serikali ibadilishe sheria ndogondogo zisizonajita kwa maendeleo ya taifa na uchumi wetu.