
Zitto baada ya kuhojiwa kwa saa zaidi ya mbili amesema kuwa ameshangazwa na hofu ya serikali dhidi ya viongozi wa vyama vya upinzani na kusema kuwa kitendo hicho nikuminya uhuru wa demokrasia.
Kwa mujibu wa Zitto Kabwe , amehojiwa kuhusu kauli alizozitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala Jijini Dar es salaam ambapo Zitto Kabwe hotuba aliyoitoa kwa mujibu wa polisi ililenga kumchonganisha Rais Magufuli na wananchi.
Amehojiwa kuhusu kusema Rais ameropoka kuhusu sakata la sukari pamoja na suala la kuwaita wanafunzi wa Dodoma vilaza ambapo Zitto alimtaka Rais awaombe wazazi na wanafunzi hao radhi kwa kuwa wazazi wa wanafunzi hao masikini ndiyo walimpigia Rais Magufuli kura.
Jeshi la polisi limesema Zitto kutumia lugha ambayo inaweza kuleta uvunjivu wa amani katika nchi Yote hayo yapo chini ya kufungu 89(1)(a) cha Penal Code " kutumia maneno ya matusi yenye kuweza kuvunja amani ya nchi.
Kabwe ameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kufika kituo cha polisi Juni 15, 2016 kwaajili ya mahojiano zaidi.