Thursday , 2nd Jun , 2016

Serikali imesema inatambua uwepo wa utaratibu wa kutozwa kodi mara mbili kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa za nje Tanzania bara kupitia Zanzibar kwa sababu ya kutokana na mifumo tofauti ya ulipaji.

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma jana Katika kipindi cha Maswali na Majibu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashantu Kijaji amesema tofauti ni Tanzania inatumia mfumo wa Import Export Commodity Databaase(IECDB), kwa ajili ya kutathimi kiwango cha kodi.

Dkt. Ashantu amesema mpango wa muda mfupi na mrefu utakaokuwa wa kdumu katika kutatua changamoto za wafanyabiashara kutozwa kodi mara mbili ni serikali ya Zanzibar kuridhia mifumo ya utahamishaji wa kodi inatumika ndani ya idara ya forodha.

Dkt. Kijaji alitoa ufafanuzi huo baada ya mbunge wa Shauri Moyo,Mattar Ali Salum, kuhoji endapo serikali inakujua kuwa kuna unatozwaji kodi mara mbili kwa wafanyabiashara na wana mpango upi wa kutatua tatizo hilo.