Wednesday , 1st Jun , 2016

Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) inalaani vikali vitendo vya mauaji ya kikatili vinavyoendelea kutokea katika maeneo mbalimbali nchini hususan mikoa ya Kanda ya Ziwa, Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bw. Bahame Nyanduga, imesema kuwa matukio haya ya ukatili yanakiuka haki ya kuishi na ni kinyume na mafundisho ya imani mbalimbali hivyo yasifumbiwe macho na kuachwa yaendelee kwani yanaweza kuleta mazoea mabaya ya kuona suala la kuua ni jambo la kawaida.

Aidha, tume inashauri Jeshi la Polisi lichukua hatua mahsusi katika kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao huku ikiwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi katika kufichua maovu na kubaini uvunjifu wa haki za binaadamu katika jamii ili kukomesha mauaji hayo.