
Aliyekuwa Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime
Mexime anatarajia kuchukua mikoba ya Adolph Rishard ambaye uongozi wa timu hiyo haujaridhishwa na kiwango chake cha kazi.
Kwa upande wa Mtibwa Sugar pia inatarajia kumrejesha aliyekuwa kocha wake Mkuu Salum Mayanga ambaye msimu uliomalizika alikuwa akiifundisha Tanzania Prisons ya jijini Mbeya ambayo ilimaliza ligi ikiwa kwenye nafasi ya nne kwa kubeba pointi 51.