Wednesday , 23rd Apr , 2014

Mbunifu wa mitindo ya mavazi maarufu hapa Tanzania, Martin Kadinda leo hii ameshiriki katika Kikaangoni Live ya ukurasa wa facebook wa EATV, na kupata nafasi ya kuchat moja kwa moja na mashabiki wake kupitia ukurasa huu.

Martin Kadinda ndani ya EATV

Martin katika nafasi hii, ameweza kuweka sawa mambo mbalimbali kumhusu yeye na kazi zake kwa mashabiki wake ambao wamekuwa na kiu ya muda mrefu kufahamu.

Enewz, baada ya kijasho cha Kikango tukaongea na Martin kuhusiana na zoezi hili zima la masaa mawili ambapo ameweka wazi kuwa amefurahi kupata nafasi hii adimu ya kuchat na mashabiki wake moja kwa moja, kitu ambacho ni kigumu kukifanya akiwa katika ukurasa wake binafsi kutokana na ratiba zake kubana na mashabiki kuwa wengi.

Endelea kuwa sehemu ya familia kubwa ya wapenzi wa ukurasa wa facebook wa EATV, shiriki ukurasa huu na marafiki na Like pia kama bado hujafanya hivyo na kumbuka, Wiki ijayo tunakuletea staa mwingine mkali ambaye utachat naye moja kwa moja.