Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama.
Waziri Muhagama amesema hayo jana wakati wa maonesho ya zana za usalama kazini yaliyofanyika Mjini Dodoma, ambapo kampuni mbalimbali zilijumuika katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya usalama mahala pa kazi kuelekea sikukuu ya wafanyakazi duniani Mei Mosi.
Aidha Waziri Muhagama, amesema sekta ambazo zina nafasi kubwa ya kutoa ajira nchi ndio zinakabiliwa na changamoto ya Usalama Mahala pa kazi lakini ndio zinazokuza uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa ikiwemo sekta ya Ujenzi
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa usalama mahala pa Kazi, Dkt. Akwilima Kayumba, amesema kuwa suala la usalama mahala pa kazi sio kwa sekta rasmi peke lakini watatoa mafunzo hata kwenye sekta ambazo sio lazima ili kuimarisha usalama wa wananchi wanapokuwa makazini.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana, amesema maandilizi yote ya maandhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo yanafanyika mjini Dodoma yameshakamilika kwa kiasi kikubwa.