Friday , 18th Mar , 2016

Chama cha Wananchi CUF kimesema kinachoendelea visiwani Zanzibar ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu hivyo kimeziomba mamlaka husika kuwaacha wananchi wa visiwa hivyo wafanye maamuzi wanayoyataka.

Naibu katibu Mkuu wa CUF, Bi. Magdalena Sakaya

Hayo yamezungumza jana na Naibu katibu Mkuu wa CUF, Bi. Magdalena Sakaya wakati akizungumzia hali ya kisiasa na uchaguzi wa marudio unavyoendelea visiwani Zanzibar.

Bi. Magdalena amesema kuwa kuna matukio ya kihalifu yanayoendelea visiwani humo wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa marudio mambo ambayo inawezekana ni mipango ya vikundi fulani ambavyo vinalenga kuharibu taswira ya visiwa hivyo.

Aidha Naibu katibu Mkuu amezitaka mamlaka husika kuzipa uzito lawama ambazo zinaelezwa kwa vyombo vya habari juu ya matukio yanayoenelea visiwani humo ili kumpa haki ya kuishi kwa amani na utulivu kila mwananchi wa visiwa hivyo.