Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas ,
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna uwepo kwa njama za watu hao kufanya tukio la Ujambazi ndipo askari hao walipofika eneo la tukio na kuweza kuzima uvamizi huo.
Kamanda Sabas amesema kuwa majambazi hayo baada ya kusimamishwa na askari wa jeshi hilo watu hao waliokuwa wamevalia makoti marefu ambayo ndani walificha silaha walianza kurushiana risasi na askari hao hali iliyopelekea kujeruhiwa kwa majambazi hayo na kufariki dunia wakati wakiwa njiani kuepelekwa Hospitali.
Aidha Kamanda Sabas amesema kuwa katika tukio hilo bunduiki mbili zimepatikana ikiwemo aina ya short gun Pumb action yenye namba za usajili L824574, ambayo iliibiwa kituo cha afya cha Tumaini.
Kamanda Sabas ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uwepo wa njama za uhalifu hali ambayo itasaidia kudhibiti matukio ya Kijambazi.