Tuesday , 8th Mar , 2016

Huduma za matibabu katika Hospitali ya Butimba Wilayani Nyamagana Mkoa Mwanza zililazimika kusimama kwa zaidi ya saa sita hapo jana kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa Hospitali hiyo kwa madai ya usalama wao mahali.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw. Baraka Konisaga.

Mgomo huo wa wafanyakazi hao umekuja ikiwa ni baada ya siku chache Hospitali hiyo kukumbwa na kashfa ya kusababisha vifo vya mama mjamzito na wanawe mapacha huku mama mwingine akipoteza wanawe wawili mapacha wakati wa kujingua.

Wakizungumza katika kikao cha pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo Kaimu Mganga mfawidhi wa hosptali hiyo Dkt. Agness Mwita na Hoseana Kusiga, ambae ni kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, wamesema watumishi wamekua wakifanya kazi katika mazingira magumu tangu matukio hayo yatokee.

Hata hivyo Mgomo huo ulimalizwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Bw. Baraka Konisaga baada ya kukutana na wafanyakazi wa hospitali hiyo na kuwaondoa hofu kwa kuwahakikishia usalama wakati wote wakiwa kazini.