Sunday , 14th Feb , 2016

Maambukizi ya Ukimwi katika mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa halmashauri ya Mbarali mkoa wa Mbeya yanaongezeka kwa mujibu ya upimaji ulio fanyika hivi karibuni katika mamlaka hiyo

Mwenyekiti Mtendaji wa Tacaids, Dokta Fatma Mrisho

Takwimu hiyo imetolewa na mwenyekiti wa mamlaka hiyo, Ayubu Chaula katika baraza la mji la kujadili mambo mbalimbali ya Mji huo ambapo kulifanyika na uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa mamlaka ambapo amesema kuwa kila watu 100 kuna watu 20 wenye maambukizi.

Mwenyekiti wa kamati ya Ukimwi, Chameta Godigodi amesema kuwa maambukizi yanapanda katika kila mwezi katika halmashauri hiyo .

Katika uchaguzi huo makamu mwenyekiti kuwa ni Godigodi alishinda kwa kupata kura 70 baada ya kumshinda kwa kura Ashery Ngowole ambaye alipata kura 27 kati ya kura 103 na kura 2 zikiharibika.