Thursday , 4th Feb , 2016

Mahakama ya hakimu Mkazi kisutu imeamuru kubomolewa kwa eneo la Kijiji cha Makumbusho ya CCM eneo la Lego Shekilango maarufu jina la 'Dagaa Dagaa' Jijini Dar es Salaam eneo lililokuwa linamilikiwa na Umoja wa Wazazi wa CCM,

Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Bulembo

na kupewa kwa mwekezaji Dar es Salaam Cul Makers LTD.

Akiongea wakati wa utekelezaji wa tukio hilo Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Bulembo amesema ubomoaji huo umekiuka taratibu kwa kuwa kesi hiyo bado haijatolewa maamuzi na mahakama kuu ambapo waliipeleka baada ya kutolewa maamuzi ya Kwanza.

Alhaj Bulembo ameongeza kuwa Licha ya kesi hiyo kuendelea lakini pia utaratibu uliotumika wa kuvnja bila kutoa notes kwa wakazi wa eneo hilo ni uonezi hivyo wamepanga jumatatu kuwasilisha tena malalamiko yao Mahakamani.

Bulembo amesema kuwa hati ya kwanza kabisa ya eneo hiyo ni ya Umoja wa wazazi wa CCM, kabla ya kuingia katika mgogoro ambao umedumu kwa takribani miaka tisa na kesi pia inaendelea katika mahakama kuu.

Kwa Upande wake wakili wa Dar es Salaam cool Makers amesema wamepata oda kutoka mahakamani na walishatoa notes miaka mingi iliyopita ili wakazi na wafanyabiashara wa eneo hilo wahame lakini hawajatekeleza.