Monday , 18th Jan , 2016

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam lawashikilia watuhumiwa watatu kwa kujihusisha na mtandao wa kuuza dawa za kulevya.

Simon Sirro

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa watatu kwa kujiusisha na mtandao wa kuuza dawa za kulevya baada ya kukamatwa na dawa hizo aina ya Heroine kilo Tisa pamoja na wengine sita wa unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Simon Simon Siro amesema amesema mbali ya watuhumiwa hao kujihusisha na dawa za kulevya pia wamekuwa wakisafirisha binadamu kwenda nchi zinazouza dawa za kulevya.

Kamanda Sirro amesema kumekuwa na ongezeko la dawa za kulevya kunatokana na kushamiri kwa mitandao ya uhalifu wa kimataifa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kamanda Siro Ameongeza kuwa kufuatia kushamiri huko, watanzania wanaosafirishwa kiharamu wamekuwa wakiwekwa rehani katika nchi hizo na wahalifu hao ili kupewa dawa za kulevya hali inayopelekea watanzania hapo kuteseka na wengine kupoteza maisha.

Kwa upande mwingne,Kamanda Siro amesema wamefanya msako na kuwakamata wahalifu sugu sita wa unyang'anyi wa kutumia silaha pamoja na magari ya wizi manne.