
Kundi la Mafikizolo likifanya mambo Mlimani City DSM
Historia imeweza kuandikwa kwa mara nyingine tena jana usiku nchini Tanzania baada ya Kundi la Muziki kutoka Bondeni Afrika Kusini la Mafizolo kudondosha show kali kwa watanzania katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar-es-Salaam na kuwaacha mashabiki wakitamani usiku huo usiishe.
Kundi hilo liliweza kumiliki jukwaa vilivyo na kupelekea mashabiki kucheza na kuimba nao nyimbo zao mbalimbali, ambapo pia katika usiku wa jana walitambulisha track yao mpya ya Nakupenda ambapo wamedokeza wanampango wa kupiga picha video ya track hiyo nchini Tanzania.
Burudani hiyo iliyotolewa na kundi hilo lenye kushikilia tuzo kadhaa barani Afrika, kwa takribani muda wa saa mbili mfululizo lilikonga nyoyo za mashabiki wao huku wakionekana kuchenguka zaidi na ngoma zao kama vile Khona, Happiness na Emlanjeni.
Madansa wa kundi hilo nao walionekana kuwa kivutio kikubwa kwa Watanzania kutokana na aina ya uchezaji wao kuwa yakipekee.