Saturday , 5th Apr , 2014

Nyota ya mwigizaji filamu wa kimataifa ambaye asili yake ni huko nchini Kenya, Lupita Nyong'o, imeendelea kung'aa zaidi, hasa baada ya mwanadada huyu kupata shavu la kuwa balozi wa bidhaa maarufu za urembo huko Marekani.

Lupita Nyong'o

Mrembo huyu katika mkataba mnono alioingia na kampuni hiyo, pia atakuwa msemaji rasmi wa bidhaa za kampuni hiyo ambayo soko lake lipo katika nchi mbalimbali duniani.

Kwa nafasi hii Lupita anakuwa kama mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika kupata mkataba na nafasi ya usemaji katika kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na masuala ya urembo, Lancôme USA.

Tags: