.jpg?itok=kZZ_i3dt×tamp=1473323149)
Akiongea na East Africa Radio/EATV Waziri Nape amesema Taarifa hizo ni za uzushi na uongo, na kuwataka mamlaka husika kuwachukulia hatua watu waliotoa taarifa za uongo.
“Hizo taarifa ni uzushi mtupu na uongo, mamlaka husika wachukue hatua, watimize wajibu wao, watumie sheria iliyopo kuwachukulia hatua”, alisema Mh. Nape Nnauye.
Mwishoni mwa wiki hii kuna taarifa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha ni taarifa kwa vyombo habari juu ya katazo la mavazi yasiyofaa kwenye mikusanyiko ya watu, hususan hospitali, maofisini, sokoni, na vyuoni.