Thursday , 24th Dec , 2015

Mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Young Africans wamelitaka Sirikisho la Soka nchini TFF na Bodi ya Ligi TPLB kupanga vizuri Ratiba.

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema, Ligi ni ngumu na inachangamoto zake lakini ratiba zimekuwa tatizo kubwa kutokana na baadhi ya timu kuwa na mapumziko ambayo kwa mashabiki yanaleta maana tofauti kisoka.

Mwambusi amesema, kunabaadi ya timu hazichezi kutokana na wakati na baadae wanakuja kucheza kama viporo ambapo wanakuwa na mapumziko ya muda mrefu tofauti na timu nyingine.

Mwambusi amesema, kama kucheza timu zote shiriki za Ligi kuu zicheze michezo yote ifanane na Ligi iishe sawa na kama kusimama basi isimame Ligi nzima ili kusiwe na viporo kwani Ligi ni ya ushindani.