Wednesday , 23rd Dec , 2015

Wazalishaji, watafiti na wakulima wa mbegu za mafuta ya kula nchini wameitaka serikali kuzuia uingizaji wa mafuta hayo kutoka nje ya nchi kwani yamekuwa yakisababisha kudorora kwa soko la mafuta.

Moja ya Mashamba ya zao la Alizeti ambalo hutumika kutengenezea mafuta nchini.

Baadhi ya wakulima na wataalam wa mbegu za mafuta wamesema asilima 51 ya mafuta yanayo tumika nchini huagizwa toka nje ya nchi hivyo kusababisha kudorora kwa soko la ndani na kushauri serikali kuwapatia mbolea za kupandia kwa wakati ili kukuza mazao ya alizeti na ufuta ambayo yamekuwa tegemeo kubwa kwa kuzalisha mafuta.

Aidha wakulima hao wamebainisha kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakililia tatizo la kuingizwa kwa mafuta kutoka nje lakini serikali imekuwa ikikaa kimya bila kufanyia kazi na kwamba mbegu nyingi zimekuwa zikifanyiwa utafiti kwa miaka mingi lakini nguvu yake huisha na kusababsha hasara.

Mwenyekiti wa chama cha wadau wa mbegu za mafuta yanayolimwa Tanzania (TEOSA) Rashid Mamu amesema asilimia 51 ya mafuta ya kula yanayo toka nje ya nchi na yamekuwa akigharamu karibu dola za kimarekani milioni 230 milioni hivyo kusababisha hasara kubwa kwa nchi.

Ameongeza kuwa maeneo ya kilimo yamejikuta yakibaki wazi na wakulima kushindwa kuchangia ukuaji wa uchumi huku wazalishaji wa mbegu kutoka mikoa ya Morogoro na Dodoma wakizungumzia changamoto ya kutoota kwa mbegu na nini kifanyike kukabiliana na hali hiyo.