Tuesday , 22nd Dec , 2015

Joh Makini ametolea ufafanuzi mitindo tofauti ya flows katika kazi zake ambayo imekuwa ikitafsiriwa tofauti hususan na wasanii wa Hip Hop wanaosimamia misingi ya fani hiyo, akieleza kuwa kufanya kazi tofauti ndio njia pekee ya msanii kupiga hatua.

Joh Makini

Joh ambaye anazishikilia chati mbalimbali ndani na nje ya mipaka ya nchi kupitia rekodi yake ya Don Bother ft AKA, amesema kuwa imefika mahali ambapo haifai tena kuendelea kufanya muziki kwa mazoea na kuweka ubunifu mbele, hili likiwa ni somo pia kwa rappers wanaotaka kufika mbali kutika game ya muziki Bongo.