Eluka Kibona, Meneja Utetezi na Ushawishi Oxfam
Wakizungumza mjini Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro wakati wa uzinduzi wa program ya majaribio ya msafara inayolenga kuibua na kuinua vipaji mbalimbali kwa vijana waliokata tamaa ya maisha vijana hao wamesema pamoja na changamoto nyingine vijana wanapoteza ndoto zao kutoka na kutumia dawa za kulevya ambapo wameishauri serikali kuanzisha operesheni maalumu ya kusaka na kuteketeza dawa hizo.
Mwakilishi wa Oxfam Tanzania, Eluka Kibona amesema shirika hilo letaendelea kuunga mkono jitihada za vijana kufikia malengo yao katika nyanja tofauti tofauti ikiwemo Kilimo Sayansi,Elimu na nyanja nyingine toafauti tofauti.
Kibona ameongeza kuwa pia wamejikita kuwasaidia watoto wa kike kwa kuzingatia kuwa idadi kubwa ya wasichana hapa nchini hukosa fursa mbalimbali kutokana na mila potofu, sera mbovu za serikali zisizozingatia usawa wa kijinsia.