Monday , 23rd Nov , 2015

Shirikisho la ngumi nchini BFT limesema, mashindano ya taifa yatasaidia kuweza kupata wachezaji watakaoongezea kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa na michuano ya kuwania kushiriki mashindano ya Olimpiki RIO 2016.

Makamu wa Rais wa BFT Wililo Lukelo amesema, mashindano ya taifa yanatarajhiwakufanyika mwanzoni mwa mwakani kwa kushirikisha mikoa mbalimbali hapa nchini.

Lukelo amesema, kikosi cha timu ya taifa ya ngumi nchini kinaendelea na maandalizi ya michuano hiyo inayopangwa na shirikisho la ngumi Afrika IBF Afrika kufanyika Machi au Aprili ambapo Tanzania iliyopo kanda ya nne kwa upande wa Bara la Afrika imepangwa na nchi nyingine za Afrika.