
Mkurugenzi mkuu wa SSRA Bi. Irene Kisaka (kushoto) akiwa na mkuu wa elimu na mawasiliano kwa umma wa mamlaka hiyo Bi. Sarah Kibonde Msika
Mkurugenzi wa Utafiti na Uendelezaji Sera wa Mamlaka hiyo Ansgar Mushi ametoa agizo hilo leo kufuatia kile alichoeleza kuwa ni mbinu chafu zinazotumiwa na mifuko ya jamii katika kupata wanachama wa kujiunga na mifuko yao.
Mushi amefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria namba nane iliyoanzisha mamlaka hiyo, ni kosa kwa waajiri kuwalazimisha wafanyakazi wao kujiunga na mifuko ambayo waajiri hao wameichagua, na badala yake wawaachie wafanyakazi wenyewe wachague mfuko wa hifadhi ya jamii ambao wanataka kujiunga.