
Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amesema licha ya kuongeza ajira kwa vijana lakini michezo ni sehemu nzuri ya utalii ambayo inaweza kuongeza pato la nchi na kuweza kuitangaza zaidi.
Bayi amesema, michezo inahitaji wawekezaji na bila kuwekeza katika michezo hatuwezi kufikia malengo ambayonchi imejiwekea kwa lengo la kukuza michezo hususani kwa vijana.