
Azam FC wataendelea kumkosa kocha wao, Muingereza Stewart John Hall siku hiyo uwanjani kwa sababu bado anatumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyooneshwa katika mchezo dhdi ya Coastal Union ambapo Stewart atasafiri na timu na kuiandaa kama kawaida mazoezini, lakini siku ya mechi atakuwa jukwaani na mashabiki wengine kuangalia mchezo.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea katikati ya wiki ambapo Yanga SC wakiwakaribisha Toto Africans Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stand United na Majimaji FC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, JKT Ruvu na Mtibwa Sugar Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Prisons na Simba SC Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Coastal Union dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumatano.
Ligi itaendelea siku ya Alhamisi ambapo Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, Mwadui FC ikimenyana na Mgambo Shooting Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wenyeji wa African Sports ya Tanga.