
Mama wa mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi wa Tanzania akiwa na mama yake marehemu Mary Thomas Ngowi
Imeelezwa kuwa mwili huo umepangwa kusafirishwa kesho ambayo ni siku ya Alhamis kwenda Moshi kwa ajili ya maziko kijijini kwake Old Moshi,Tela Mande.
Shughuli za msiba kwa sasa zinaendelea nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea 'Kwa Mama Ngowi ambapo kutakuwa na Misa ya kumuombea Marehemu sambamba na zoezi la kutoa heshima za mwisho leo hii jioni na vilevile kesho katika kanisa la mtakatifu Joseph lililopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
eNewz inatoa pole na kuwatakia faraja ndugu, jamaa, marafiki na kila anayeguswa na msiba huo kwa namna moja ama nyingine, na tunaitakia roho ya marehemu mapumziko mahala pema peponi, Amin.
