Friday , 2nd Oct , 2015

Nyota wa muziki wa nchini Uganda, Jose Chameleone, Moze Radio & Weasel, Bebe Cool, na Rema kati ya wengine wengi, wameunganisha nguvu zao kutoa sapoti kwa maandalizi ya kampeni za kugombea urais, wakiwa nyuma ya rais Yoweri Museveni.

Nyota wa muziki wa nchini Uganda, Jose Chameleleone akiwa na Rais Yoweri Museveni

Katika muunganiko huo wa kuekelea uchaguzi mkuu mwaka kesho, kivutio kikubwa katika tukio hilo ni nyota Bebe Cool na msanii Rema Namakula ambaye alikuwa chini yake kuonyesha ukaribu mkubwa ambao umemaliza kabisa uvumi wa kuwepo kwa ugomvi kati ya pande hizo mbili toka walipoacha kufanya kazi pamoja.

Wasanii wengine ambao wameonesha kuwa mstari wa mbele katika shughuli hiyo wakiweka pembeni tofauti zote zilizokuwepo baina yao pia ni Mun G, Moze Radio vilevile King Saha, ikiwa ni sehemu tu ya orodha ya mastaa inayokuwa.

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanaona urafiki huo wa wasanii ni mkakati wao kujivunia mapesa kutokana na tetesi ya kutengwa kwa fungu la kutosha kwa ajili yao katika safari hiyo ya kampeni.