Wednesday , 9th Sep , 2015

Kocha wa Timu ya Mgambo Shooting Bakari Shime amesema timu yake itazindua harakati zake za Ligi kuu ya Soka Bara kwa kunyakua pointi tatu muhimu dhidi ya Ndanda Fc kwani wanaamini usajili walioufanya pamoja na mazoezi ndio ngao yao.

Kikosi cha Timu ya Mgambo Shooting ya jijini Tanga

Shime amesema, hafikirii kupoteza mchezo huo kwani anaamini wachezaji wake wamejiandaa vizuri zaidi ya mwaka jana ambapo waliweza kuwashinda wakiwa nyumbani.

Shime amesema Ndanda ni timu ya kawaida na hawezi kufikiria kama wataweza kupoteza katika mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Shime amesema kuanza Ligi kwa ushindi ni kitu kizuri kwa sababu kinasaidia kuongeza morali ya wachezaji na ndio sababu kubwa ya kupania kupata matokeo mazuri kwa kutambua umuhimu huo.