Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
Akiongea na Wagaga wakuu wa mikoa na Wilaya pamoja na Wauguzi katika mkutano wa Mkuu Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amesema miongoni mwa mambo mengine ambayo serikali ya awamu ya nne imefanikiwa ni pamoja na ongezeko la vituo 3619 hadi 7247 mwaka 2015.
Mh. Bilal ameongeza kuwa licha ya mafanikio hayo katika Sekta ya Afya lakini Tasnia hiyo inakubwa na changamoto mbalimbali ikiwemo malalamiko mengi yanayoelekezwa kwa watendaji wa afya.
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal amewataka watumishi wa afya nchini kuendelea kuelimisha jamii juu ya namna ya kujikinga na maradhi mbalimbali ili jamii iondokane na maradhi ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu unaotishia maisha ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwa sasa.
Dkt. Bilal ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa mwaka wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya sambamba na kutoa vyeti kwa wataaalamu wa afya walioshiriki kutoa huduma kwa wagonjwa wa Ebola nchini Liberia na Sierra Leone.
Awali katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa sekta ya Afya nchini Tanzania na Kimataifa wakizunguimzia mafaniko ya sekta hiyo kwa sasa wamesema ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na watoto, kupunguza maambukizi ya Ukiwi na Kifua Kikuu.

