Monday , 7th Sep , 2015

Mtunzi mahiri wa filamu Tanzania Daniel Manege amenuia kuonesha umuhimu wa elimu na changamoto zake, kupitia filamu ya SAFARI YA GWALU mwishoni mwa mwezi huu, ikibeba kisa cha kijana aliyeamua kurudi shule ya msingi baada biashara yake kufeli.

Mtunzi mahiri wa filamu Tanzania Daniel Manege

Msisimko zaidi katika kazi hiyo unaletwa na wasanii walioteka soko kwa sasa Gabo Zigamba, Cheche wa siri ya Mtungi na Rachel kati ya wengine, inakuwa ni kazi ya aina yake ambayo itadhihirisha kukua kwa soko la filamu kwa mujibu wa mtunzi mahiri wa filamu Tanzania Daniel Manege.