Katikia taarifa yake, mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Mtwara Athumani Kambi, amesema mchezo huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Ndanda huku wakiwa na lengo ka kuwatambulisha wachezaji wapya.
Kambi amesema, amesema juhudi zinafanyika ili kuhakikisha kuanzia msimu mpya wa ligi kuu itakapoanza wawakilishi wa vilabu hawataruhusiwi kukusanya mapato mlangoni katika uwanja huo na baadala yake kutakuwa na utaratibu mwingine ambao utatangazwa, ili kudhibiti upotevu wa mapato.
