Katibu wa kongamano la Baraza la Wanawake wa kiislamu Wilaya ya Kongwa Mariam Issa Msami.
Wito huo umetolewa katika kongamano la Baraza la Wanawake wa kiislamu Wilaya ya Kongwa Dodoma ambapo Katibu wake Mariam Issa Msami amesema kukua kwa demokrasia kunalifanya taifa kukabiliwa na changamoto ambazo zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu huku
Aidha Bi, Mariamu ametoa wito kwa vijana kuwa makini katika maamuzi ya kupata viongozi wenye weledi wa kuliongoza taifa.
kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kongwa, Bituni Msangi aliyealikwa kwenye kongamano hilo amewataka wanawake kuacha kuwa tegemezi badala yake wajiunge kwenye vikundi vya uzalishaji mali na biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kibaigwa Richard Kapinye ametoa wito kwa kinamama kuwarithisha watoto mafundisho ya dini ili kuwajengea maadili mema ya makuzi.