Monday , 22nd Jun , 2015

Baada ya kuchukua tuzo na Wimbo wao wa Walewale, Band ya Muziki wa Dansi Vijana Ngwasuma wamesema wataachia nyimbo mbili kwa mpigo baada ya Ramadhani ikiwa kama zawadi kwa mashabiki wao.

Vijana wa Ngwasuma

Akiongea na eNews Mmoja wa Wanamuziki wa Kundi hilo Toscanee Maziwa amesema kuwa nyimbo hizo ambazo wataziachia moja wameipa jina la Mama Afrika na nyingine ni Karibu.

Toscanee amesema baada ya kuachia nyimbo hizo wataachia Album yao ambayo ipo mbioni kumalizika na wameipa jina la Wale Wale.